- Aliyekuwa jaji mkuu wa humu nchini, Willy Mutunga hatimaye amelizungumzia kuhangaishwa kwa Ndii, Wanjigi na Miguna
- Pia, Mutunga alizungumzia hatua ya Matiang'i kuidharau na kuipuuzilia mbali idara ya mahakama
Jaji Mkuu wa zamani, Willy Mutunga mnamo siku ya Alhamisi, Aprili 12 alijitokeza kuchangia kuhusu kuhangaishwa kwa wakosoaji wakuu wa serikali ndani ya muungano wa NASA, hasa Miguna Miguna.
Habari Nyingine: Jamaa apeana mkewe kwa mwenzake kwa wiki moja baada ya kupoteza 'pata potea' ya soka
Alisema kuwa alihuzunika na kufedheheka kwa matukio kadha ya hivi punde humu nchini, ambayo kulingana naye, yanairudisha taifa katika enzi za ukoloni.

Habari Nyingine: Gavana Mutua amdhihirishia mkewe kuwa ndiye bora kuliko wote, amwonyesha makuu ya dunia
Akihojiwa katika NTV, Mutunga aliishtumu serikali kwa jinsi ilivyoshughulikia kesi za Miguna, Ndii na Wanjigi, hata baada ya mahakama kuipa mwelekeo.
"Kilichowafanyikia Miguna, Ndii na watu kama Wanjigi kupoteza paspoti zao kilinihuzunisha sana kwa sababu haya ndiyo yaliyofanyika mika aya 70s na 80s," Alisema Mutunga.
Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

Habari Nyingine: Binti alalamika baada ya kufukuzwa kanisani kwa "kuvaa vibaya" (picha)
Alikariri kuwa hakuna Mkenya yeyote anayeweza kupoteza uraia wake alioupata kwa kuzaliwa.
" Uhuru wa kutembea hauna pingamizi. Na hata kama unachukua paspoti ya mtu, ni lazima umwambie ni kwa nini," Aliendelea kuzungumza.
Kando na kuhangaishwa kwa watatu hao, Mutunga aliivamia serikali kwa kutotii idara ya mahakama hasa kutokana na tetesi za Matiang'i dhidi ya majaji.

Habari Nyingine:
"Huwezi kupewa notisi na mahakama kisha usema hukupewa nafasi ya kusikizwa na hukwenda. Unaona anavyozungumza na unashangaa ni nani anayemshauri," Alisema Mutunga.
Read ENGLISH VERSION
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdibH5xfZNmoqKkmZi1sMPAn5insZmgtqJ5zKKerqaRYsSiusminqJlnpZ6r7DIomSkoZyeu6q%2FyKSgraGjna5uw8ilo7JlnarBtrrGmmWhrJ2h